*STORI*:*MTUMWA MWAMINIFU
*MWANDISHI*:KELV CHITANDA
*SEHEMU YA 1*
Jakson alijikuta anakuwa mtumwa wa mapenzi baada ya kuwa katika mahusiano na msichana mmoja ambaye ukimwangalia kwa jicho la kawaida unaweza kusema hakuwahi kutembea na mvulana yeyote, ni kwa vile alivyokuwa mtulivu lakini kumbe alikuwa jamvi la wageni. Hivyo Jackson kumpenda Irene ilikuwa ni sawa na kupoteza tu muda wake. Yaani ilikuwa ni sawa na kumwandikia mtu meseji I LOVE YOU alafu unasubiri majibu wakati sio swali.
*** ***
Hata hivyo Jackson aliishia kuumia kutokana na mwendendo wa Irene, yote yalidhoofisha moyo wa Jackson hapo ndipo Jackson alipobaini kuwa 'si kila kinga'aacho ni dhahabu'. Hata hivyo licha ya hayo yote Irene aliigiza kuwa mwema kwa Jackson katika hali ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa, lakini Jackson hakufahamu kuwa ni bora ukweli utakaomtoa machozi kuliko uongo utakaoumiza maisha yake. Irene alijitahidi kuwa na Jackson ili aweze kupata chapaa kutoka kwa kwa Jackson hivyo hakuwa na Upendo wa dhati zaidi ya tamaa ya pesa.
*** ***
Siku moja Jackson alijaribu kukaa na Irene, walijadili mengi sana yanayohusu mahusiano yao na maisha kwa ujumla, upepo uliwabembeleza kwa sauti mzuri.
"Nikuulize kitu Irene?"
Aliuliza Jackson, hata hivyo Irene alionekana kuwa na mawazo mengi sana kama ilivyokawaida pale mtu anapoambiwa 'Baby nikuulize kitu?"
"Niulize tu"
"Hivi ni kwanini mapenzi yetu iwe sababu ya mimi kuumia na kuteseka..........?"
(Kabla hajamaliza)
"Eeh....jamani kwanini mpenzi kwanini uumie?"
"........kuwa makini na hisia za mwenzako kwenye mapenzi, usimwambie mtu nakupenda kwa kumdanganya ili tu ukidhi haja zako, kuwa mwaminifu kwenye mahusiano, usimpotezee mtu muda wake......heshimu hisia za binadamu mwenzio....!"
"Eeh haya jamani nimekuelewa"
Irene alikubali japo kwa shingo upande akiamini hana dosari yeyote katika penzi lao kwani ingawa Jackson aliamini kuwa kusamehe ni mwanzo wa maisha mapya kiasi cha kuchukua uamuzi wa kumsamehe Irene lakini kumbe Irene alifanya kuondoa ngoma juani hivyo hali na mwenendo wa Irene ulibaki kuwa kama wa zamani, ndipo Jackson alipobaini kuwa kubadili tabia ya Irene ni sawa na kuondoa chuvi kwenye maji ya bahari kwani 'kivuli cha fimbo hakimfichi mtu miale ya jua'
*** ***
Hata hivyo licha ya kubaini kuwa kuvumilia tabia ya Irene katika mapenzi yao ni kupoteza muda, Jackson hakufahamu kuwa kipi ni bora kati ya kufanya anachofikiri au afikiri anachofanya hivyo Jackson alibaki kuwa mtumwa mwaminifu katika penzi ilo.
*** ***
Ama kweli hakuna hesabu ngumu kama kumtoa mwanamke kwenye kiti hadi kitandani, Mussa alibaini ilo baada ya kuwa katika mahusiano na Esha lakini changamoto ikawa ni kuhusu kukutana faragha kwani ingawa wote walipendana kwa dhati lakini kulikuwa na vikwazo vilivyowazuia kucheza ule mchezo wa kikabila.
Hata hivyo Mussa hakuvunjika moyo wala mguu bali alikuwa tayari kusubiri hadi pale mambo yatakapokuwa sawa ili waweze kucheza huo mchezo wa kikabila. Yote tisa kumi ni kwa sababu Esha alikuwa anasoma hivyo waliishia kupeana imani tu kuwa ipo siku watakutana faragha kucheza mchezo huo bila matatizo yeyote.
"Tuendelee kusubiri, one day yea........"
"Mmh okay poa, lakini tafadhali kusubiri isiwe sababu ya kuniumiza!"
"Hapana jamani sikuumizi niamini please!"
"Nitashukuru dear"
"Usijali"
Hivyo mapenzi ya Mussa na Esha yalidumu kwa muda mrefu kwani waliweza kuelewana kwa jila jambo tena mengi yalikuwa ni siri yao wakiamini 'Wapishi wengi uharibu mchuzi'. Hayo yote yalikuwa tofauti kwa mapenzi ya Jackson na Irene yaliyokuwa yamekosa mwelekeo kama ndege iliyopoteza dira na kujikuta inaelekea baharini. Yote ni kwa sababu Irene alijikita zaidi kwenye pesa sio mapenzi ya dhati kama ilivyotegemewa na Jackson hivyo Jackson aliumizwa zaidi kiasi cha kuwa Mtumwa wa mapenzi hata akakosa hamu ya kupenda tena.
*** ***
Licha ya kuwa mbali na Irene kwani Jackson alikuwa anaishi kijiji cha Majengo wakati huo Irene alikuwa ni mwenyeji wa kijiji cha Juhudi, Jackson hakuwahi kupokea japo meseji kutoka kwa Irene mpenzi wake, Irene alimtumia meseji mpenzi wake pale alipokuwa na shida ya haraka.
Siku moja Jackson akapokea SMS kutoka kwa Irene, meseji ambayo hqta kabla hajaifungua Jackson alifahamu fika lengo la kutumwa kwa meseji hiyo, alipoifungua ilisomeka hivi;
"BABY , NINA SHIDA YA ELFU 30 YA SALOON JAMANI"
Hapo sasa Jackson alipokata shauri na mapenzi hayo yaliyojikita zaidi kwenye fedha, Jackson alimkumbuka shairi la 'Your lost' alichokuwa amekisoma wakati yuko kidato"
"Hivi Irene utaacha link dharau wewe mwanamke, yaani wewe ndiyo wakuniandikia mierufi mikubwa hiyo, umenionq mimi kipofu?, asa nasema hivi kuanzia leo mimi na wewe basi tusijuane ....mpuuzi mmoja wewe"
Hadi hapo inaoneaha wazi kuwa ni mwisho sasa wa mapenzi ya Janickson na Irene, Jackson aliona kama vile ametoka kifungoni ingawa Irene hakuwa ridhaa kabisa kwani wiki moja aliyokaa bila mahusiano na Jackson kwake ilikuwa ni kama karne moja na miongo mitatu, yaani aliwaza sana, hayo yote ni kwa sababu alishazoea kupata hela kila alivyokuwa anaomba, sasa mambo yalikuwa ni kinyume kwani mahuasono yao ni sasa mafuta na maji.......................!
Na huu ndiyo mwisho wa sehemu hii ya kwanza karibu katika sehemu nyingine zijazo upate kujua hatima ya mapenzi ya Jackson na Irene wananiambia.........!!
No comments:
Post a Comment